SOMO LA 1
Siku
moja Jimi alimwuliza mtu mmoja anayekana kuwa kuna Mungu endapo alipata
kujaribu sana, hata kwa dakika chache tu, kupigana na wazo lisemalo
kwamba huenda Mungu yuko.
"Sawa
kabisa!" mkana Mungu yule akajibu, akimwacha Jimi na mshangao.
"Miaka mingi iliyopita, mimi nilikuwa karibu sana nigeuke na kuwa
mtu anayemwamini Mungu. Nilipokiangalia kile kiumbe kidogo sana - lakini
- kikamilifu katika kitanda chake kidogo,
nilipochungulia na kuviona vidole vile vidogo fahamu za kwanza za kutambua, nilipita katika kipindi cha miezi kadhaa ambayo katika hiyo mimi nilikuwa karibu kabisa niache kuwa mkana Mungu. Kule kumwangalia mtoto yule kulikuwa kumenishawishi karibu kabisa kuwa hapana budi Mungu alikuwa yuko."

1.
Kila Kitu Kilichobuniwa Kina Mbunifu Wake
Muundo
wa mwili wa kibinadamu unafanya iwepo haja ya kuwako mbunifu wake. Wanasayansi
wanatuambia kwamba ubongo wetu hukusanya na kukumbuka picha elfu nyingi
katika mawazo yetu, huyaunganisha matatizo yetu yote na kuyatatua, hufurahia
kuona uzuri, huitambua nafasi ya mtu, na kutaka kukuza yaliyo bora ndani
ya kila mtu. Chaji za umeme zitokazo katika ubongo huongoza shughuli
zote za misuli ya miili yetu.
Kompyuta
pia zinafanya kazi kwa njia ya mikondo ya umeme. Lakini ilichukua akili
ya mwanadamu katika kuitengeneza hiyo kompyuta na kuiambia la kufanya.
Si
ajabu, basi, kwamba mtunzi wa Zaburi alihitimisha kwa kusema kwamba
mwili wa mwanadamu unasimulia habari za Muumbaji huyo wa ajabu kwa sauti
kubwa iliyo wazi:
"Nakusifu maana nimefanywa kwa namna ya ajabu, matendo yako ni ya ajabu, wewe wanijua kabisa kabisa" - (Zaburi 139:14)
"Nakusifu maana nimefanywa kwa namna ya ajabu, matendo yako ni ya ajabu, wewe wanijua kabisa kabisa" - (Zaburi 139:14)
Hatuna
haja ya kwenda mbali ili kuyaona hayo "matendo" ya Mungu.
Umbo la ubongo wetu wenye sehemu nyingi za ajabu na viungo vyetu vingine
ni "matendo" ya Mungu, nayo husonda kidole chake kwa yule
mbunifu stadi kabisa.
Hakuna
pampu yoyote iliyotengenezwa na mwanadamu inayoweza kulinganishwa na
moyo wa mwanadamu. Hakuna mtandao wo wote wa kompyuta uwezao kuwa sawa
na mfumo wetu wa mishipa ya fahamu. Hakuna mfumo wo wote wa Televisheni
unaofanya kazi yake vizuri kama sauti, sikio, na jicho la mwanadamu.
Hakuna kiyoyozi kikuu cho chote (central air conditioning) wala mfumo
wa kuipasha joto nyumba uwezao kushindana na kazi inayofanywa na pua,
mapafu, na ngozi yetu. Mfumo wenye sehemu nyingi za ajabu wa mwili wa
mwanadamu unadokeza kwamba mtu fulani alihusika katika kuubuni, na Mtu
huyo fulani ni Mungu.
Mwili
wa mwanadamu ni mfumo kamili wa viungo mbali mbali - vyote vikiwa vinashirikiana,
vyote vikiwa vimeumbwa kikamifu. Mapafu na moyo, mishipa ya fahamu na
misuli, hiyo yote hufanya kazi za ajabu mno kiasi cha kuwa vigumu kusadikika
ambazo hutegemezwa juu ya kazi nyingine zilizo za ajabu mno kiasi cha
kutufanya sisi tushindwe kusadiki.
Endapo
ungetakiwa kuzipa nambari sarafu kumi kuanzia moja mpaka kumi, na kuziweka
mfukoni mwako, na kuzitikisa-tikisa huku na huku, kisha kuzitoa mfukoni
mwako na kuziweka tena mfukoni moja moja, je, kuna uwezekano gani kwamba
ungefanya hivyo kwa kufuata mfuatano wa nambari zake sawa sawa? Kwa
sheria ya mahesabu unayo bahati moja tu katika bilioni kumi ya kuzitoa
kwa mpangilio wake kuanzia ya kwanza mpaka ile ya kumi.
Sasa,
basi, hebu fikiria ni bahati ngapi tumbo la chakula, ubongo, moyo, ini,
arteri, vena, figo, masikio, macho, na meno vingekuwa nazo vikikua vyote
pamoja na kuanza kufanya kazi yao kwa dakika ile ile ya wakati mmoja.
Hivi
maelezo ya busara kabisa ni yapi kuhusu ubunifu huo wa mwili wa mwanadamu?
"Kisha
Mungu akasema, 'Natumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu,'..............Hivyo
Mungu Akamwuumba Mtu Kwa Mfano Wake,...... mwanamume na mwanamke aliwaumba"
- (Mwanzo 1:26,27).
Mwanaume
na mwanamke wa kwanza wasingeweza kuwa wametokea wenyewe tu. Biblia
inathibisha kwamba Mungu alitubuni sisi kwa mfano wake. Alituwaza katika
mawazo yake na kutuumba.
2.
Kila Kitu Kilichoumbwa Kina Muumbaji Wake
Lakini
ushahidi wa kuwako kwake Mungu haufungamani tu na ubunifu wa miili yetu;
pia umetandaa huko mbinguni. Acha taa za mjini, angalia juu katika mbingu
ya usiku. Wingu lile jeupe kama maziwa lenye nyota, tunaloliita Mkanda
wa Nuru (Milky Way) ambalo kwa kweli ni kundi la mabilioni ya majua
(galaxy) yanayotoa mwanga mkali wa moto sawa na ule wa jua letu ambao
unaweza kuonekana hapa duniani kwa kupitia katika darubini kubwa zilizopo
hapa duniani kama ile darubini iitwayo "Hubble Telescope"
iliyo katika anga za juu.
Si
ajabu, basi, kwamba mtunga Zaburi alihitimisha kwa kusema kwamba nyota
zinamtangaza Muumbaji Mtukufu:
"Mbingu zatangaza utukufu wa Mungu, anga ladhihirisha kazi ya mikono yake" (Zaburi 19:1-3).
"Mbingu zatangaza utukufu wa Mungu, anga ladhihirisha kazi ya mikono yake" (Zaburi 19:1-3).
Je,
hivi sisi twaweza kutoa hitimisho gani la busara kwa kuangalia mpangilio
huo unaotatanisha sana na ukubwa wa malimwengu yote?
"Hapo
mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi" (Mwanzo 1:1).
"Yeye
[Mungu] alikuwako kabla ya vitu vyote; vyote hudumu mahali pale kwa
uwezo wake" (Wakolosai 1:17).
Viumbe
vyote humshuhudia yule Mungu Mbunifu Mkuu na Muumbaji asiye na Mwisho.
Katika maneno haya rahisi, "Hapo mwanzo Mungu," tunalipata
jibu la siri ile ya uhai. Yuko Mungu aliyeumba kila kitu.
Wanasayansi
wakuu wengi siku hizi wanamwamini Mungu. Dk. Arthur Compton, mwanafizikia
mshindi wa tuzo ya Nobel, akitoa maoni yake juu ya fungu hilo la Maandiko,
siku moja alisema hivi:
"Kwangu binafsi, imani huanza ninapotambua kwamba yule aliye na akili isiyo na kifani ndiye aliyeyaweka hayo malimwengu na kumwumba mwanadamu. Kwangu mimi si vigumu kuwa na imani hii, kwa maana ni dhahiri kwamba po pote pale palipo na mpango yupo Mungu mwenye akili. Malimwengu yaendayo kwa utaratibu, na kujifunua kwetu hushuhudia ukweli wa usemi huu adimu mno uliopata kunenwa - 'Hapo mwanzo Mungu'"

Biblia
haijaribu kumthibitisha Mungu inatangaza kuwako kwake. Dk. Arthur Conklin,
mwana biolojia, siku moja aliandika hivi: "uwezekano kwa uhai kutokea
kwa ajali ni sawa na uwezekano kwa kamusi kamili kutokea kutokana na
mlipuko katika kiwanda cha kuchapisha vitabu".
Twajua
kwamba wanadamu hawawezi kutengeneza kitu cho chote bila kutumia kitu
kingine. Twaweza kujenga vitu, kuvumbua vitu, kuunganisha vitu, lakini
kamwe hatujapata kufanya kitu cho chote bila kuwa na kitu kingine cha
kuanzia, awe ni chura mdogo kabisa ua la kawaida kabisa. Vitu vituzungukavyo
pande zote hupiga kelele vikisema Mungu ndiye aliyevibuni, Mungu ndiye
aliyeviumba, Mungu ndiye anayevitegemeza. Jibu pekee linaloaminika kuhusu
chimbuko la malimwengu hayo, dunia hii, na wanadamu - ni Mungu.
3.
Mungu Huingia Katika Mahusiano Na Watu Binafsi
Mungu
yule aliyezibuni mbingu hizo na nyota, aliyeyaumba malimwengu hayo,
anatafuta kuwa na uhusiano nasi binafsi. Alikuwa na uhusiano wake binafsi
na Musa: "Bwana akasema na Musa....kama vile mtu asemavyo na rafiki
yake" (Kutoka 33:11). Mungu Mwenyewe anataka kuingia katika uhusiano
nawe na kuwa Rafiki yako. Yesu aliwaahidi wale wanaomfuata, akisema
"Ninyi mmekuwa rafiki zangu" (Yohana 15:14).
Sisi
sote tumeshughulika sana na wazo hilo la Mungu, kwa kuwa wanadamu kwa
asili wanapenda dini. Hakuna mnyama yeyote ajengaye madhabahu kwa ajili
ya ibada. Lakini kila mahali unapowakuta wanaume na wanawake, unawakuta
wakiabudu. Ndani ya kila moyo wa mwanadamu kuna ufahamu kuwa Mungu yuko,
tamaa ya kuwa rafiki wa Mungu. Tunapoitikia hiyo tamaa yetu na kumpata
Mungu, hatuwi na mashaka tena juu ya kuwako kwake na hitaji letu.
Katika miaka ile ya 1990 mamilioni ya wanaomkana Mungu katika nchi ya Urusi waliachana na imani yao hiyo ya kumkana Mungu, kisha wakamgeukia Mungu. Profesa wa Chuo Kikuu cha St. Petersburg alitoa kauli yake inayofanana na maoni yaliyotolewa na wakana Mungu wengi katika Umoja wa Kisovieti iliyopita:
"Nimetafuta maana ya maisha katika utafiti wangu wa kisayansi, lakini sikuona kitu chochote cha kutegemea. Wanasayansi wanaonizunguka mimi wanazo hisia hizo hizo za ukiwa. Nilipoangalia ukubwa wa malimwengu katika somo langu la elimu ya nyota, kisha nikaangalia ukiwa uliomo moyoni mwangu, niliona kwamba ni lazima pawe na maana fulani. Kisha nilipoipokea Biblia uliyonipa na kuanza kuisoma, ukiwa katika maisha yangu ukajazwa. Nimeiona Biblia kuwa ndiyo chimbuko la pekee la matumaini kwa nafsi yangu. Nimempokea Yesu kama Mwokozi wangu, nami nimepata amani ya kweli pamoja na kuridhika katika maisha yangu".
Mkristo anamwamini Mungu kwa sababu yeye amekutana naye na kugundua kwamba anayatosheleza mahitaji makubwa sana ya moyo wake. Mungu ambaye Wakristo wamemuona kuwa yuko, anatupatia mtazamo mpya, maana mpya, makusudi mapya na furaha mpya.

hatuahidi sisi kwamba tutakuwa na maisha yasiyo na taabu, wala mapambano,
ila yeye anatuhakikishia kwamba atatuongoza na kutusaidia kama tutakuwa
na uhusiano binafsi naye. Na mamilioni ya Wakristo wanaweza kutoa ushuhuda
wao kwamba ingekuwa heri kwao kuacha kila kitu kuliko kuyarudia maisha
yale yasiyokuwa na Mungu.
Hii
ndiyo ajabu kuu kuliko zote kwamba yule Mungu Mwenyezi aliyeyabuni,
aliyeyaumba na kuyategemeza malimwengu hayo anataka kufanya uhusiano
na kila mwanaume na mwanamke, kila mvulana na msichana. Daudi alishangaa
sana kuhusu jambo hilo alipoandika maneno haya:
"Nikiangalia mbingu, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota ulizozimika huko, mtu ni nini ee Mungu hata umfikirie mwanadamu ni nini hata umjali?" - (Zaburi 8:3,4).
"Nikiangalia mbingu, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota ulizozimika huko, mtu ni nini ee Mungu hata umfikirie mwanadamu ni nini hata umjali?" - (Zaburi 8:3,4).
Muumbaji
wetu ana "mjali" kila mmoja wetu. Yeye binafsi anakupenda
sana wewe kana kwamba wewe ulikuwa ni kiumbe chake cha pekee alichokiumba.
Basi
tunaweza kumwamini Mungu:
(1) Kwa sababu ya ubunifu wake wenye sehemu nyingi katika kila kitu alichokiumba ambacho kinatuzunguka sisi.
(2) Kwa sababu shauku ile iliyomo ndani yetu juu ya Mungu inatufanya tusiwe na raha mpaka tupatapo pumziko letu ndani yake tena.
(3) Kwa sababu tunapomtafuta na kumpata, Mungu hutosheleza kila haja tuliyo nayo pamoja na shauku yetu - kikamilifu!

4.
Ni Mungu Wa Aina Gani?
Ni
jambo la busara tu kwamba Mungu aliye na nafsi yake apende kujifunua
mwenyewe kwa viumbe wake kama vile baba atakavyo watoto wake wamjue.
Na katika Biblia Mungu anatuambia yeye ni nani, tena anafananaje.
Ni
mfano gani alioutumia Mungu katika kuwaumba wanaume na wanawake?
"Hivyo
Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba"
(Mwanzo 1:27).
Kwa
kuwa sisi tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, basi, uwezo wetu wa kufikiri
na kujisikia, kukumbuka na kutumaini, kutafakari na kuchambua mambo
- chimbuko lake lote latoka kwake. Je, tabia kuu ya Mungu ni ipi?
"Mungu
ni upendo" (1 Yohana 4:8).
Mungu
hufanya uhusiano wake na wanadamu kutokana na moyo wake wa upendo. Hakuna
kitu cho chote alichofanya au atakachopata kufanya ambacho hakijasababishwa
na upendo wake usio na ubinafsi, ujitoao mhanga.
5.
Jinsi Yesu Anavyotufunulia Alivyo Mungu
Katika
Biblia Mungu anarudia tena na tena kueleza habari zake Mwenyewe kwamba
Yeye ni Baba.
"Je!
Sisi sote si watoto wa baba mmoja"?
"Je, sisi sote hatukuumbwa na Mungu yule yule?" Malaki 2:10.
"Je, sisi sote hatukuumbwa na Mungu yule yule?" Malaki 2:10.
Baadhi
ya mababa tuwaonao leo si cho chote, bali hawapendezi. Kuna mababa wasiojali,
mababa wanaotukana matusi. Mungu si kama hao. Yeye anajali, ni Baba
anayeguswa sana na mambo yetu. Ni Baba apendaye kucheza na mwanawe au
binti yake, ni Baba anayewafurahisha sana watoto wake kwa kuwasimulia
hadithi kabla hawajaenda kulala usiku.
Baba
yetu huyo mwenye upendo alitaka kufanya zaidi ya kule kujifunua Mwenyewe
kwa njia ya maneno ya Maandiko. Alijua kwamba yule mtu tunayeishi naye
ni mtu halisi kuliko yule tunayesikia tu habari zake au tunayesoma habari
zake. Kwa hiyo yeye akaja katika dunia yetu kama mtu halisi - yaani,
yule mtu Yesu.
"Kristo
mfano wa Mungu asiyeonekana" - (Wakolosai 1:15).
Basi
kama wewe umemwona Yesu, utakuwa umemwona Mungu. Alijishusha hadhi yake
na kuwa sawa sawa na sisi akawa kama sisi - ili apate kutufundisha jinsi
ya kuishi na kuwa na furaha, ili kwamba sisi tupate kuona jinsi Mungu
alivyo hasa. Yesu ni Mungu aliyeonekana kwa macho. Yeye mwenyewe alisema,
"Aliyeniona mimi amemwona Baba" (Yohana 14:9).
Usomapo
kisa cha Yesu katika vitabu vinne vya Injili, yaani, vitabu vinne vya
kwanza vya Agano Jipya, utagundua picha ya kuvutia sana ya Baba yetu
aliye mbinguni. Wavuvi wale wa kawaida tu walizitupa nyavu zao ili kumfuata
Yesu, na watoto wadogo wakasongamana kwenda kwake kupokea baraka zake.
Aliweza, kumfariji mwenye dhambi aliyeharibika kabisa na kuzivunja nguvu
za mnafiki sugu aliyejihesabia haki yeye mwenyewe. Aliponya kila maradhi
kuanzia upofu hadi ukoma. Katika matendo yake yote Yesu alidhihirisha
kwamba Mungu ni upendo! Alikidhi haja ya mwanadamu kwa namna ambayo
hakuna mtu ye yote aliyepata kufanya hivyo kabla yake au tangu wakati
wake!
Ufunuo
wa Yesu wa mwisho ambao unaonyesha utukufu wa jinsi Mungu alivyo ulitokea
pale msalabani.
"Kwa
maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee,
ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele"
- (Yohana 3:16).
Yesu
alikufa sio tu kutupatia maisha yenye furaha sasa, bali kutupa uzima
wa milele pia. Kwa vipindi virefu watu walishangaa, na kutumaini, na
kuota
ndoto juu ya Mungu. Waliiona kazi ya mikono yake mbinguni na katika uzuri wa viumbe vya asili. Kisha pale msalabani, Yesu alikivunjilia mbali kimya cha vizazi vingi, na watu wakajikuta wanautazama ana kwa ana uso wa Mungu, wakimwona yeye kama alivyo hasa - yeye ni upendo, wa milele, tena ni upendo udumuo milele!
Wewe
waweza kumgundua Mungu sasa hivi Yesu anapomfunua kwako. Ugunduzi huo
utakufanya utoe uthibitisho wako binafsi, ukisema: "Baba, nakupenda!"ndoto juu ya Mungu. Waliiona kazi ya mikono yake mbinguni na katika uzuri wa viumbe vya asili. Kisha pale msalabani, Yesu alikivunjilia mbali kimya cha vizazi vingi, na watu wakajikuta wanautazama ana kwa ana uso wa Mungu, wakimwona yeye kama alivyo hasa - yeye ni upendo, wa milele, tena ni upendo udumuo milele!
Kama una maoni au maswali au unahitaji kusoma kozi hii ya masomo ya Biblia tafadhali andika kisha tuma kwenye anuani ya Barua pepe mpandasdachurch@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni