Jumamosi, Oktoba 11, 2014

MIKUTANO MIKUBWA YA UAMSHO KATIKA MJI WA MPANDA.

Kanisa la Waadventista wa Sabato mitaa ya MPANDA na Kakese imekubaliana kufanya mikutano ya uamsho
Chini ya Wachungaji wa mitaa hiyo, Mchungaji wa mtaa wa MPANDA Pr.AMOS YARAGWILLA na Mchungaji wa mtaa wa Kakese Pr. LAMECK MANIGINA. Mikutano hiyo inafanywa na makanisa 4 yaliyo katika mji wa Mpanda. Aidha mikutano hiyo inafanywa kwa mzunguko, yaani makanisa yote kukusanyikia kwenye kanisa moja na na kufanya ibada. Jumamosi iliyopita tarehe 4/10/2014 ibada ilifanyikia katika kanisa la Mpanda mjini, jumamosi hii ya tarehe 11/10/2014 ibada inafanyikia kanisa la Kawajense,  sabato ya  tarehe 18/10/2014 ibada itafanyikia kanisa la Kichangani. Sabato ya  tarehe 25/10/20 ibada ni katika kanisa la Kashaulili, Sabato ya tarehe 1/11/2014 ibada itafanyikia maeneo ya Kigamboni iliyo chini ya kanisa la Mpands mjini na Kigamboni inakusudiwa kufunguliwa Kundi na baadae kidogo litatengwa kuwa kanisa. Mikitano hii hufanyika siku mbili kwa kila kituokituo yaani jumamos siku nzima na jumapili kuanzia saa kumi jioni

Hakuna maoni:

MPANDA SDA CHURCH