Kanisa la Waadventista wa Sabato ulimwenguni kote litakuwa na siku kumi za kufunga na kuomba. Mfungo huo utaanza jumatano tarehe 07/01/2015.
Lengo la mfungo huo ni kujiweka kwa MUNGU katik kipindi hiki cha nyakati za mwiaho pamoja na kuomba kumwagwa kwa Mvua ya masika "ROHO MTAKATIFU" kwa ajili ya kumaliza kazi ya utume ulimwenguni. Katika kanisa la Waadventista wa Sabato Mpanda mjini mkoani Katavi washiriki wameaswa kuhudhuria. Mchungaji wa mtaa wa Mpanda amesisitiza washiriki kuhudhuria na kwamba washiriki wote watakusanyika kanisani kwa ajili ya somo maalum na maombi kila siku saa 11:30 alfajiri na saa 11:00 jioni kila siku kwa muda wa siku kumi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni