Jumapili, Februari 15, 2015

WATU 13 WAMKIRI YESU KWA NJIA YA UBATIZO KATIKA MAHUBIRI YA SATELLITE KANISA LA MPANDA SDA

MPANDA: Mahubiri ya Satellite yaliyokuwa yanarushwa na kituo cha televisheni ya kanisa la Waadventista wa Sabato Tanzania

Morning star Tv, yamemalizika kwa kishindo katika kanisa la Waadventista wa Sabato Mpanda mjini mkoani Katavi. Mahubiri hayo
yaliyokuwa yanaendeshwa na makamu mwenyekiti wa kanisa la Waadventista wa Sabato duniani mchungaji Geoffrey Mbwana. Mahubiri hayo yaliyoanza tarehe 24 january yamemalizika jana 14 february 2015. Katik
a kilele cha mahubiri hayo, watu 13 wamemkiri Yesu kwa njia ya ubatizo

Mchungaji wa mtaa wa Mpanda Pr.AMOS YARAGWILLA akibatiza watu waliojitoa wakati wa mahubiri ya Satellite

Ubatizo huu ulifanyikia katika kisima cha ubatizo kilicho katika viwanja  vya kanisa la Waadventista wa Sabato Mpanda mjini. Muda mfupi kabla ya ubatizo kisima kilionekana kujaa maji hadi juu na ikalazimika kupunguza maji hayo.

Kisima kikiwa kimejaa maji









Hakuna maoni:

MPANDA SDA CHURCH