SOMO LA 2.
Baada ya kusoma na kumaliza somo la kwanza, sasa karibu katika somo la pili lisemalo "TWAWEZA KUIAMINI BIBLIA"
Mabaharia
waasi maarufu walioizamisha meli ya Kiingereza iliyoitwa Bounty waliishia
kufanya makazi yao wakiwa pamoja na wanawake, wenyeji wa eneo lile katika
kisiwa cha Pitcairn katika Bahari ya Pasifiki ya Kusini. Kundi lile
lilikuwa mabaharia tisa wa Kiingereza, wanaume wa Kitahiti sita, wanawake
wa Kitahiti kumi, na msichana wa miaka kumi na mitano. Mmojawapo wa
mabaharia wale alivumbua namna ya kutonesha [kugeuza kuwa mvuke] alkoholi,
na baada ya muda mfupi ulevi ukaliharibu koloni lile lililokuwa katika
kisiwa kile. Ugomvi kati ya wanaume na wanawake ukageuka na kuwa wa
kutumia nguvu.
Baada
ya kupita muda fulani mmoja tu kati ya wanaume wale wa kwanza waliofika
mle kisiwani ndiye alibaki kuwa hai. Lakini mtu huyo, Alexander Smith,
alikuwa ameigundua Biblia katika mojawapo la makasha yaliyochukuliwa
kutoka katika ile meli. Alianza kuisoma na kuwafundisha wengine juu
ya kile ilichosema. Alipofanya hivyo maisha yake yeye mwenyewe yakabadilika
na hatimaye maisha ya wote waliokuwa katika kisiwa kile.
Wakazi
wa kisiwa kile walikuwa wametengwa na ulimwengu wa nje mpaka ilipowasili
meli ya Kimarekani iliyoitwa Topaz katika mwaka wa 1808. Wafanyakazi
katika meli hiyo wakakikuta kisiwa kile kikiwa na jumuia inayokua na
kusitawi, bila ya kuwa na pombe kali (wiski), gereza, wala uhalifu.
Biblia ilikuwa imekigeuza kisiwa kile kutoka jehanamu ya duniani kwenda
katika kielelezo cha vile Mungu atakavyo ulimwengu huu uwe. Na mpaka
leo hii kinaendelea kuwa katika hali hiyo.
Je,
hivi Mungu bado anaendelea kusema na watu kupitia katika kurasa hizo
za Biblia? Bila shaka anafanya hivyo. Ninapoandika haya, naliangalia
karatasi la majibu lililotumwa kwetu na mwanafunzi mmojawapo wa kozi
zetu za Biblia. Maelezo chini yake yanasema hivi "Mimi nimo gerezani,
niko katika orodha ya watu wanaostahili kunyongwa, nimehukumiwa kufa
kwa kutenda kosa la jinai. Kabla ya kuchukua kozi hii ya Biblia, nilikuwa
nimepotea lakini sasa ninacho kitu cha kutumainia tena nimeupata upendo
mpya."
Biblia
inao uwezo unaoweza kuyabadilisha kabisa maisha ya watu. Kwa kweli,
watu wanapoanza kujifunza Biblia, maisha yao hubadilika kwa namna ya
kuvutia sana.
1.
Jinsi Mungu Anavyozungumza Nasi Kupitia Katika Biblia
Baada
ya kumwumba Adamu na Hawa, yaani, yule mwanaume na mwanamke wa kwanza
wa duniani, Mungu alizungumza nao uso kwa uso. Lakini Mungu alipokuja
kuwatembelea baada ya wao kutenda dhambi, je, wale watu wawili walifanya
nini?
"Mwanaume yule na mkewe wakasikia sauti ya BWANA Mungu alipokuwa akitembea mle bustanini wakati wa jua kupunga, nao WAKAJIFICHA ASIWAONE BWANA MUNGU katikati ya miti ya bustani." (Mwanza 3:8).
"Mwanaume yule na mkewe wakasikia sauti ya BWANA Mungu alipokuwa akitembea mle bustanini wakati wa jua kupunga, nao WAKAJIFICHA ASIWAONE BWANA MUNGU katikati ya miti ya bustani." (Mwanza 3:8).
Dhambi
ilikata mawasiliano ya ana kwa ana kati ya mwanadamu na Mungu. Baada
ya dhambi kuingia katika ulimwengu huu, je, Mungu aliwasilianaje na
watu?
"Hakika
Bwana Mwenyezi hafanyi kitu, bila kuwafunulia watumishi wake manabii
nia yake." - Amosi 3:7.
Mungu
hakutuacha sisi gizani kuhusu maisha haya tuliyo nayo na maana yake.
Kupitia kwa manabii wake - yaani, watu wale aliowaita Mungu kuwa wanenaji
na waandishi wake - wamefunua majibu yake kwa maswali makuu yahusuyo
maisha yetu.
2.
Ni Nani Aliyeiandika Biblia?
Manabii
waliutoa ujumbe wa Mungu kwa kutumia sauti na kalamu zao katika kipindi
chao walichoishi, na walipokufa, maandiko yao yaliendelea kuwapo baada
yao. Kisha ujumbe huo wa manabii ulikusanywa pamoja chini ya uongozi
wake Mungu, na kuwekwa katika kitabu tunachokiita Biblia.
Lakini
maandiko yao hayo yanaaminika kwa kiasi gani?
"Zaidi ya hayo, lakini kumbukeni kwamba hakuna mtu ye yote awezaye kufafanua mwenyewe unabii ulio katika Maandiko Matakatifu. Maana hakuna ujumbe wa kiunabii unaotokana na matakwa ya binadamu bali watu walitoa unabii wakiongozwa na Roho Mtakatifu" (2 Petro 1:20,21).
"Zaidi ya hayo, lakini kumbukeni kwamba hakuna mtu ye yote awezaye kufafanua mwenyewe unabii ulio katika Maandiko Matakatifu. Maana hakuna ujumbe wa kiunabii unaotokana na matakwa ya binadamu bali watu walitoa unabii wakiongozwa na Roho Mtakatifu" (2 Petro 1:20,21).
Waandishi
wa Biblia waliandika si kwa kufuata mapenzi au tamaa yao, bali kama
walivyoongozwa au kuvuviwa na Roho wa Mungu. Biblia ni kitabu cha Mungu!
Katika
Biblia hiyo Mungu hutuambia habari zake Mwenyewe, tena hutufunulia makusudi
yake aliyo nayo kwa ajili ya wanadamu. Inaonyesha mtazamo wa Mungu kwa
mambo yale yaliyopita, kisha inatufunulia mambo ya mbele, ikitueleza
jinsi tatizo la uovu litakavyotatuliwa mwishoni na jinsi amani itakavyokuja
katika dunia yetu.
Je,
hivi Biblia yote ni ujumbe utokao kwa Mungu?
"Maandiko yote, Matakatifu yameandikwa kwa uongozi wa Mungu, na yanafaa kuonya, kusahihisha makosa yao, na kuwaongoza, katika kufundishia ukweli, mtu wa Mungu awe mkamilifu na tayari kabisa kufanya kila kazi njema, waishi maisha adilifu" - (2 Timotheo 3:16,17).
"Maandiko yote, Matakatifu yameandikwa kwa uongozi wa Mungu, na yanafaa kuonya, kusahihisha makosa yao, na kuwaongoza, katika kufundishia ukweli, mtu wa Mungu awe mkamilifu na tayari kabisa kufanya kila kazi njema, waishi maisha adilifu" - (2 Timotheo 3:16,17).
Biblia
Takatifu huyabadilisha kabisa maisha ya wanadamu kwa sababu Biblia "yote"
ina "pumzi ya Mungu," ni hati iliyovuviwa, ni kitabu cha Mungu.
Manabii walisimulia kile walichokiona na kukisikia kwa kutumia lugha
ya wanadamu, lakini ujumbe wao ulitoka moja kwa moja kwa Mungu. Kwa
hiyo, ukitaka kujua maisha haya yana maana gani, soma Maandiko Matakatifu.
Kuisoma Biblia kutayabadilisha kabisa maisha yako. Kadiri unavyozidi
kuisoma kwa maombi, ndivyo utakavyozidi kupata amani moyoni mwako.
Roho
Mtakatifu yule yule aliyewavuvia manabii kuandika, Biblia hiyo, atayafanya
mafundisho ya Biblia, injili yake, ifae kuyabadilisha kabisa maisha
yako ukimwalika Roho kuwapo wakati unapoisoma hiyo Biblia.
3.
Umoja wa Biblia
Kwa
kweli Biblia ni maktaba ya vitabu 66. vitabu 39 vya Agano la Kale viliandikwa
kuanzia karibu na mwaka wa 1450 K.K hadi 400 K.K, Vitabu 27 vya Agano
Jipya viliandikwa kati ya mwaka wa 50 B.K na mwaka wa 100 B.K.
Nabii
Musa alianza kuandika vitabu vitano vya kwanza wakati fulani kabla ya
mwaka wa 1400 K.K. Mtume Yohana alikiandika kitabu cha mwisho cha Biblia,
yaani, kitabu cha Ufunuo, karibu na mwaka wa 95 B.K. Katika kipindi
cha miaka 1,500 kati ya kuandikwa kitabu cha kwanza na cha mwisho cha
Biblia, walau watu wengine wapatao 38 waliovuviwa walitoa mchango wao.
Wengine walikuwa wafanya biashara, wengine wachungaji wa kondoo, wengine
wavuvi, wengine askari, matabibu, wahubiri, wafalme - wanadamu toka
katika tabaka zote za maisha. Mara nyingi waliishi katika utamaduni
na falsafa vilivyohitilafiana.
Lakini
hapa ndipo yalipo maajabu ya maajabu yote: Vitabu hivyo 66 vya Biblia
pamoja na sura zake 1,189 zenye idadi ya mafungu 31,173 vikiwekwa pamoja,
tunaona umoja na mwafaka katika ujumbe vinaoutoa.
Hebu
na tuseme kwamba mtu mmoja anagonga mlangoni pako, halafu anapokaribishwa
ndani, anaweka kipande cha marumaru chenye umbo la ajabu juu ya sakafu
ya chumba chako cha kuongea, halafu anaondoka bila kusema neno lo lote.
Wageni wengine wanamfuata, mmoja baada ya mwingine, mpaka takribani
watu 40 wanaweka kila mmoja kipande chake cha marumaru mahali pake.
Wa
mwisho anapokwenda zake, kwa mshangao wewe unaona jengo zuri limesimama
mbele yako. Ndipo wewe unajifunza kwamba sehemu kubwa ya "mafundi
hao wanachonga mawe" hawajawahi kuonana kamwe, wakiwa wamekuja,
kama walivyofanya, kutoka Amerika ya Kusini, China, Urusi, Afrika na
sehemu nyingine za ulimwengu.
Je,
wewe ungeamua nini? Ya kwamba mtu fulani alipanga umbo hilo lililojengwa
kwa mawe ya kuchonga naye alimtumia kila mtu vipimo sahihi kutokana
na kipande chake kile kimoja cha marumaru.
Biblia
nzima inatoa ujumbe mmoja unaoshikamana - sawasawa tu na lile jengo
la mawe yaliyochongwa ya marumaru. Mtu fulani mmoja mwenye akili alipanga
yote hayo, yaani, ni akili za Mungu. Umoja wa kushangaza wa Maandiko
Matakatifu unatoa ushahidi wake kwamba ingawa ni wanadamu walioyaandika
mawazo yale, yalikuwa yamevuviwa naMungu.
4.
Waweza Kuiamini Biblia
1.
Kuhifadhiwa kwa Biblia ni jambo la ajabu sana. Maandiko yote ya awali
ya Biblia yalinukuliwa kwa mkono - muda mrefu kabla ya kuwako
mitambo ya kuchapisha vitabu. Waandishi wale walitayarisha nakala za maandiko ya mkono ya asilia na kuzitawanya. Maelfu ya nakala kama hizo za maandiko ya mkono au sehemu zake bado ziko mpaka sasa.
mitambo ya kuchapisha vitabu. Waandishi wale walitayarisha nakala za maandiko ya mkono ya asilia na kuzitawanya. Maelfu ya nakala kama hizo za maandiko ya mkono au sehemu zake bado ziko mpaka sasa.
Maandiko
ya mkono ya Kiebrania yanayorudi nyuma hadi ule mwaka wa 150 mpaka 200
kabla ya Kristo yalipatikana karibu na Bahari ya Chumvi mnamo mwaka
1947. Ni jambo la kushangaza sana kwamba magombo hayo mawili yenye umri
wa miaka elfu mbili yanazo kweli zile zile tunazozikuta katika Agano
la Kale la Biblia zinazochapishwa siku hizi. Huu ni ushahidi wenye nguvu
unaoonyesha jinsi Neno la Mungu linavyoaminika.
Mitume
waliandika kwanza sehemu kubwa ya Agano Jipya kama nyaraka walizozituma
kwa makanisa ya Kikristo yaliyoanzishwa baada ya kifo na ufufuo wake
Kristo. Zaidi ya maandiko ya mkono 4,500 ya Agano Jipya lote au sehemu
yake yanapatikana katika nyumba za Makumbusho na maktaba za Ulaya na
Amerika. Baadhi yake yanakwenda nyuma hadi karne ile ya pili. Kuyalinganisha
maandiko hayo ya mkono ya awali na biblia ya siku hizi, twaweza kuona
kwa urahisi kwamba kwa kawaida Agano Jipya limeendelea pia kubaki bila
mabadiliko yo yote tangu lilipoandikwa kwa mara ya kwanza.
Siku
hizi Biblia au sehemu zake zimetafsiriwa katika lugha zaidi ya 2,060
na (dialects). Ni kitabu kinachouzwa sana ulimwengu: zaidi ya Biblia
milioni 150 na sehemu za Biblia huuzwa kila mwaka.
2.
Usahihi wa Biblia kihistoria ni wa kushangaza sana. Uvumbuzi mwingi
wa elimu ya mambo ya kale (akiolojia) umethibitisha kwa namna ya kuvutia
sana usahihi wa Biblia. Wanahistoria wamevigundua vibao vya udongo wa
mfinyanzi pamoja na majengo ya kumbukumbu ya mawe ambayo yameonyesha
majina, mahali, na matukio yaliyojulikana kuhusu siku za nyuma kutokana
na Biblia tu.
Kwa
mfano, kulingana na Mwanzo 11:31, Ibrahimu na familia yake "wakatoka
wote katika Uru... waende katika nchi ya Kanaani." Kwa kuwa ni
Biblia peke yake iliyosema juu ya Uru, mabingwa fulani wa Biblia walisema
kwamba mji kama huo ulikuwa haujapata kuwako kamwe. Ndipo wachimbaji
wa mambo ya kale wakagundua mnara wa hekalu katika nchi ya Iraki Kusini
ukiwa na kwenye msingi wake iliyoandikwa katika maandishi ya kikabari
yaliyokuwa na jina la Uru. Ugunduzi wa baadaye ulionyesha kwamba Uru
ulikuwa ni mji mkuu ambao ulikuwa unasitawi wenye ustaarabu wa hali
ya juu uliokuwa umefikiwa. Sura ya mji ule ilikuwa imesahaulika ni Biblia
peke yake iliyolihifadhi jina lake - mpaka pale koleo ya mwanaakiolojia
mmoja ilipouthibitisha ukweli wa kuwako kwake. Na huo Uru ni mmoja tu
miongoni mwa mifano mingi ya akiolojia inavyothibitisha usahihi wa Biblia.
3.
Kutimia kwa usahihi kabisa kwa utabiri wa Biblia hukuonyesha wewe kwamba
unaweza kuitegemea Biblia. Maandiko hayo yana utabiri mwingi wa kushangaza
sana wa matukio ya siku za usomi ambayo hivi sasa yanaendelea kutimia
mbele ya macho yetu. Tutauchunguza baadhi ya unabii huo wa kusisimua
katika masomo ya mbele.
5.
Jinsi Ya Kuielewa Biblia
Unapolichunguza
Neno la Mungu, weka kanuni hizi mawazoni mwako:
1.
Jifunze Biblia ukiwa na moyo wa maombi. Ukiyaendea Maandiko Matakatifu
kwa moyo na mawazo yaliyofunguliwa kwa maombi, yatageuka na kuwa mawasiliano
kati yako na Yesu (Yohana 16:13-14).
2.
Soma Biblia kila siku. Kujifunza Biblia kila siku ni ufunguo wa kupata
nguvu katika maisha yetu, ni kukutana na mawazo ya Mungu (Warumi 1:16).
3.
Unapoisoma, iache Biblia ijieleze yenyewe. Uliza: mwandishi huyu wa
Biblia alikusudia kusema nini? Kwa kuzingatia kile limaanishacho fungu
hilo, twaweza kuitumia kwa akili katika maisha yetu ya leo hii.
4.
Soma Biblia kwa kufuata somo. Linganisha andiko na andiko. Yesu alitumia
mbinu hii kuthibitisha kwamba yeye alikuwa ndiye Masihi:
"Akaanza kutoka Musa na Manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe."
"Akaanza kutoka Musa na Manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe."
5.
Jifunze Biblia ili kupokea uwezo wa kuishi kwa ajili ya Kristo. Neno
la Mungu limeelezwa katika Waebrania 4:12 kama upanga mkali ukatao kuwili.
Ni zaidi ya maneno tu yaliyo juu ya ukurasa, ni silaha iliyo hai mikononi
mwetu ya kupigia na kuyaondolea mbali majaribu yale yanayotushawishi
kutenda dhambi.
6.
Sikiliza Mungu anapozungumza nawe kupitia katika Neno lake. Endapo mtu
anataka kuujua ukweli wa Bilbia juu ya somo fulani, basi, ni lazima
awe tayari kufuata yale inayofundisha (Yohana 7:17), sio yale anayofikiri
mtu fulani, au yale yanayokaziwa na fundisho lolote la kanisa lake.
6.
Biblia Yaweza Kubadilisha Maisha Yako
"Kuyafafanua
maneno yako [Mungu] kwatia nuru, kunampa ufahamu mjinga" - (Zaburi
119:130).
Kujifunza
Biblia kutauimarisha "ufahamu" wako, kutakupa nguvu ya kuyashinda
mazoea yale yaletayo madhara, na kukuwezesha kukua kimwili, kiakili,
kimaadili na kiroho.
Biblia
inazungumza na moyo. Inashughulika na mambo yale yanayowapata wanadamu
katika maisha yao - yaani, upendo, ndoa, uzazi na kifo. Inaliponya jeraha
lenye kina kirefu sana katika tabia ya mwanadamu, pamoja na dhambi na
taabu inayotokana nayo.
Neno
la Mungu si kitabu cha jamii moja, kizazi kimoja, taifa moja, au utamaduni
mmoja. Japokuwa liliandikwa katika nchi ya Masharikiya kati, linawavutia
pia wanaume na wanawake wa Magharibi. Linaingia katika nyumba za wanyonge
na katika majumba makubwa ya matajiri. Watoto wanazipenda hadithi zake
zinazosisimua. Mashujaa wake wanawavutia sana vijana. Wagonjwa, wanaoishi
katika hali ya upweke, na wazee wanagundua ndani yake faraja na tumaini
la kuwa na maisha bora.
Kwa
kuwa Mungu anafanya kazi yake kupitia katika Biblia, basi, inao uwezo
mkubwa. Inaivunjavunja hata mioyo iliyofanywa migumu dhidi ya hisia
zote za kibinadamu, inailainisha na kuijaza na upendo. Tumeona Biblia
ikimbadilisha haramia wa zamani na mvuta bangi na kumfanya mhubiri aliye
motomoto. Tumeona Biblia ikimbadilisha mwongo na mdanganyaji na kumfanya
kuwa mwalimu mwaminifu na mwenye kuheshimika. Tumeona kitabu hicho kikiwanyakua
watu wakiwa karibu na kujiua wenyewe na kuwapa tumaini la kuanza maisha
upya. Biblia inaamsha upendo miongoni mwa maadui. Inawafanya wenye majivuno
kuwa wanyenyekevu, na wachoyo kuwa wakarimu. Biblia inatutia nguvu tunapokuwa
dhaifu, inatuchangamsha tunapokuwa katika hali ya kukata tamaa, inatufariji
tunapokuwa na huzuni, inatuongoza tunapochoka sana. Inatuonyesha jinsi
ya kuishi kwa ujasiri na jinsi ya kufa bila hofu.
Kitabu
hicho cha Mungu, yaani, Biblia kinaweza kuyabadilisha maisha yako! Utagundua
hivyo kwa dhahiri zaidi na zaidi, kadiri unavyoendelea kujifunza miongozo
hii ya GUNDUA.
Kwa
nini Biblia hiyo iliandikwa kwa ajili yetu? Yesu anatoa jibu: "Lakini
hizi [kweli za Biblia] zimeandikwa; ili mpate kuamini ya kwamba Yesu
ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini muwe na uzima kwa jina
lake" - (Yohana 20:31).
Sababu
kuu kuliko zote kwa nini sisi tunapaswa kuyafahamu Maandiko Matakatifu
ni kwamba yamejaa picha zinazomfunua Yesu Kristo na kutuhakikishia sisi
uzima wa milele. Kwa kumtazama Kristo katika Biblia nzima, tunabadilika
na kufanana naye zaidi. Basi, kwa nini wewe usianze sasa kugundua uwezo
huo wa Neno la Mungu uwezao kukufanya wewe kufanana zaidi na Yesu?
Kama una maoni au maswali usisite kutuandikia barua pepe mpandasdachurch@gmail.com au mpanda.adventist@yahoo.com pia waweza kutoa maoni/comments na kuacha mawasiliano yako hapo.
Maoni 2 :
Hakika ni somo zuri sana Mungu atusaidie na awasaidie watu wote ili waweze kuiamini Biblia, maana huwezi kumwamini Mungu au kumjua Mungu kama huiamini na kusoma Biblia kwani Mungu amefunuliwa kupitia Maandiko matakatifu yaani BIBLIA
Ubarikiwe Mtu wa MUNGU!!
Chapisha Maoni