Jumatano, Januari 21, 2015

MKUTANO MKUBWA WA INJILI TANZANIA NZIMA SASA KUANZA 24JANUARY.

Ule mkutano mkubwa wa Injili uliokuwa umepangwa kufanyika Tanzania nzima kuanzia january 11 hadi january 31 kwa njia ya Satellite kupitia televisheni ya kanisa la Waadventista wa Sabato sasa utaanza tarehe 24 january hadi 14 february.


 Katika mkutano huo kanisa la Waadventista wa Sabato Mpanda mjini limejipanga kwa ajili ya kurusha mahubiri hayo. Kanisa limejipanga kwa kununua na kurekebisha mitambo ya kupokea na kurushia mahubiri hayo. Pia limejipanga kwa kununua vitabu kwa ajili ya kuwagawia wageni watakaohudhuria katika mahubiri hayo. Pia idara yaawasiliano ya kanisa hilo imejipanga vizuri katika Mahubiri hayo ikiwa ni pamoja na kutoa matangazo ya mkutano huo pamoja na kuyarekodi mahubiri hayo. Ikumbukwe kwamba mahubiri hayo yataendeshwa katika makanisa yote ya Waadventista wa Sabato nchini kote. Katika mji wa Mpanda kutakuwa na vituo 4 katika makanisa ya Mpanda mjini, Kichangani, kashaulili na Kawajense. Mhubiri Makamu wa mwenyekiti wa kanisa la Waadventista wa Sabato ulimwenguni Pr. GEOFREY G. MBWANA. Washiriki wote wa kanisa tunapaswa kuhudhuria kila siku pamoja na wageni. TUENDELEE KUUOMBEA MKUTANO HUO.

Hakuna maoni:

MPANDA SDA CHURCH