Siku kumi za kufunga na kuomba katika kanisa la Waadventista wa Sabato Mpanda mjini zimemalizika kwa kishindo
Mfungo huo ulioanza jumatano ya tarehe 7 januari umemalizika jumamosi tarehe 17 januari 2015. Ilikuwa ni program ya aina yake iliyoambatana na waimbaji wa kwaya ya kanisa (maranatha) kikundi cha Marejeo Singers, kikundi cha Raise and Shine pamoja na vikundi vingine vya uimbaji na watu binafsi kumsifu Mungu kwa njia ya nyimbo. Program hizo zilizoanza saa 7 mchana hadi saa 1 jioni ziliambatana na shuhuda mbalimbali toka kwa washiriki wakishuhudia juu ya kile Mungu alichowatedea katika maisha yao pamoja na kile Mungu alichowatendea katika siku hizi kumi za kufunga na kuomba.Kipindi hiki kilikuwa kizuri na chenye kusisimua kwani katika visa na shuhuda hizi toka kwa washiriki zilionyesha ukuu na uweza wa Mungu jinsi anavyowatendea watu wake. Pia program hiyo iliambatana na maombi. Watu zaidi ya 100 waliofunga walikuwepo katika hitimisho la siku hizo kumi za kufunga na kuomba kubwa zaidi ikiwa ni kuomba kumwagwa kwa Roho Mtakatifu.SIFA NA UTUKUFU NI KWA MUNGU
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni